Dibaji:

Fikra ya kuunda shirikisho la Afrika ya Kusini mwa Sahara imejadaliwa kwa upana katika kongamano na mikutano ambayo walishiriki wanazuoni kutoka AFrika mikutano iliofanyika ndani na nche ya Bara la Afrika; bali fikra hii imekuwa maudhui ya gumzo na mjadala baina ya wanzuoni wa Afrika kupitia mawasiliano na mazungumzo baina yao; kama bado mawasiliano na vikao hivyo bado vinaendelea punde ikatoka kwa hali ya kwa fikra ikawa mradi ulio simama; kwa sababu nyingi matukio ya haraka katika Ulimwengu huu wa leo; Ulimwengu wa makundi na ushirikiano.

Sehemuya kwanza: Uanzishwaji na ufafanuzi

Kifungo [1] Kutoka na neno la Mwenyezi Mungu Mtukufu:
(Mwenyezi Mungu ameshuhudia kwamba hakuna mwabudiwa isipokuwa Yeye tu – na Malaika na wale wenye elimu nao pia wameshuhudia vivyo hivyo – Msimamizi wa haki; Hakuna mwabudiwa isipo kuwa Yeye tu, Mwenye nguvu, Mwenye hekima.) {Aali Imraan aya ya 18}a vile vile neno lake Mtukufu: (Kwa yakini hilo ni kundi lenu, lililo kundi moja tu, na Mimi ni Mola wenu, kwa hiyo Niabuduni) {Al anbiyaa aya ya 92} na neno la Mtume wake : ( Hakika ya wanazuoni ni warithi wa manabii)
Na kuamini umuhimu wakuunganisha juhudi na nguvu katika kufanikisha malengo na kuzuia hatari na kukabilianana changamoto.
Na vile vile kulingana na hali halisi ya ikilimi na kimataifa.

Na kutokamana na yaliozingatiwa:

• Ukosefu wa marejeo ya kielimu ya waisilamu barani Afrika.
• Ukosefu wa sauti ya kuwatetea waisilamu katika masuala ya umma na matatizo.
• Uwepo wa matatizo na mizozano ambapo waisilamu wanahusika pande moja au pande zote mbili.
• Ufarakano wa juhudi za walinganizi wa dini na ushirikiano duni baina yao.
• Udhaifu wa ilimu katika kutoa fatwa.

Kuambatana na maamuzi ya kamati andalizi, Umoja wa Wanazuoni wa Afrika ulianzishwa tarehe 7/4/1432H sambamba na 12/3/2011AD kwa muda usiojulikana.
.

Kifungo [2] Umoja wa wanazuoni wa Afrika ni chombo huru cha kiisilamu chenye kinachotambulika katika Sheria; wanakusanyika chini yake wanachama kutoka na wanazuoni wa bara la Afrika kusini mwa Sahara Kuu.
Kifungo [3] Makao ya umoja wa wanazuoni wa Afrika yako katika Jiji la Bamako nchini Mali; na yawezekana yakahamishwa katika mji wowote uleo barani Afrika baada ya kupatikana idhini kutoka kwa mkutano mikuu, na vile vile inaruhusiwa kuanzisha matawi mingine majimboni na mikowani ndani ya mipaka ya bara la Afrika kwa idhini ya bodi ya wadhamini.

Kifungo [4] Alama ya Umoja wa wanazuoni:

Ramani ya bara la Afrika yenye rangi ya kijani kibichi juu yake alama ya mnara juu ya mnara alama ya mwezi.
Sehemuya pili: Njia, Sera na Malengo na Mbinu:
Kifungo [5] Kazi ya umoja wa wanazuoni inakua katika mifumo ifuatayo:
1. Kurejea kwa Quran na Sunnah kulingana na walivyo fahamu ya maimamu wa uongofu uliosimama kwa misingi ya wasatiya.
2) uimarishaji wa mwelekeo wa ndani wa Umoja wa Afrika katika suala la uanzilishi na usimamizi na uwakilishi wa kweli wa pande zote barani.
3) uhuru na kuwa mbali na wosia.
4) kiungo karibu na jamii kupitia uhamasishaji wa nafasi ya wanachama katika mirengo ya kitaifa yenye mienendo inaofanana.

4) Kuthibiti Fatwa katika masuala ya Umma barani Afrika.
5) Kukuza mushikamano amani kati ya spectra ya jamii za kiafrika.
6) kufungua uhusiano na njia mwingiliano na jamii nyingine za Kiislamu katika masuala ya Umma wa Waislamu.
Kifungo [7] Umoja unatumia ili kufikia malengo yake njia halali; na unalenga hasa kwa hatua ya kwanza njia zifuatazo:
1) Kuratibu juhudi za kielimu, daawa na tarbiya katika bara hili.
2) Kuanzisha miradi ya kielimu, daawa na tarbiya na kuikuza.
3) Kuendeleza na kusaidia mashirika ya kiislamu nchini na katika iklimu
4) Kutoa taarifa juu ya masuala ya umma na kuzisambaza kupitia vyombo vya habari.
5) Kutoa ushauri na mwongozo na ushauri nasaha kwa wale wanaozihitaji.
6) Kufanya juhudi ya ushawishi katika utatuzi wa migogoro ambamo mna pende husika ya kiislamu.
7) Kutoa fatwa katika masuala ya umma na matukio mapya.
8) Kuamsha ujumbe wa msikiti na kuwajenga wasimamizi wake.
9) Kuanda amikutano na kongamano za kielimu na daawa na kuandaa semina na mihadhara ya umma.
10) Kuandaa kozi za mafunzo ili kujenga uwezo na kukuza vipaji.
11) Kuanzisha benki ya data za Uislamu katika Afrika ili kuwezisha kufanya utafiti muhimu.
12) Kuandaa utafiti na masomo na kuzisambaza.
13) Kuzalisha baramiji za redio na video katika lugha rasmi na kitaifa katika bara hili.
14) Kuanziasha na kutumia vyombo vya habari vya aian zote.

Sehumu ya Tatu: Uwanachama

Kifungo [8] Uanachama wa Umoja huu ni wazi kwa wanazuoni raia wa nchi za Afrika zilizo ukanda wa kijiografya uliangaziwa katika kifungo [2]
Kifungo [9] Yanazingatiwa masharti yafuatayo katika maombi ya uanachama:
a) Kuwa mwanchuoni anaejua Sheria ya kiislamu na anaelewa mabo leo na mwenye kuzingatia mazingiara na hali
b) Kuwa mtu mwenye ushawishi katika mazingiara yake.
c) Asiwe mtu anaejulika kuwa mpotofu.
Kifungo [10] Uanachama wa Umoja kwa wanachama wasio waanzilishi wapatika kwa njia zifuatazo:
– Kuwasilisha maombi ya anaetaka uwanachama kwa Afisi ya Katibu MKuu.
– Udhamini wa ngalau wawili wa wanachama waanzilishi.
– Kuridhia kwa kamati ya uanachama
– Kupitishwa kwa ridhaa katika Bodi ya Wadhamini.
Kifungo [11] Kamati ya uanachama yaweza kuwateua wale inaowaowataka kuwaita miongoni ya wanzuoni wanaotimiza masharti ya kujiunga na Umoja; na inazingatiwa ridhaa ya maandhishi kutoka kwa mpendekezwa kuwa ombi la kujiunga.
Kifungo [12] Ni haki ya vyama na mashirika ya misaada ya kiislamu kuomba kujiunga na Umoja kwa sharti ya kuwakilishwa na mtu anaetimiza masharti ya uanachama kwa mujibu ya makubaliano baina ya Umoja na mamlaka husika.
Kifungo [13] Aina ya uanachama:
a) Uanachama anzilishi; unapewa kwa waliojiunga na Umoja kabla ya Mkutano wa Uzinduzi.
b) Uanachama wa kawaida; unapewa waliojiunga na Umoja baada ya Mkutano wa Uzinduzi.
c) Uanachama wa Uangalizi; unapewa watu na taasisi ya kielimu na mashirika ya kiislamu yanaoshugulika na Afrika kutoka nche ya mfumo wa kijiografia wa Umoja.
d) Uanachama wa heshima; unapewa kwa watu mashuhuri kwa huduma yao Uislamu katika Afrika; iwe ndani au nche ya bara.
Kifungo [14] Uanachama wa Umoja ni wa kudumu; isipokuwa hupetezwa kwa kujiuzulu au kifo au kupokonya kwa mujibu wa uamuzi wa Bodi ya Wadhamini uliopitishwa katika Mkutano Mkuu.

Sehemu ya Nne: Muundo wa Shirika wa Umoja

Kifungo [15] Muundo wa Shirika wa Umoja unajuisha almashauri za daraja la juu na vyombo tendaji:
a) Almashauri za daraja ya juu
1- Jumuiya kuu
2- Mkutano Mkuu
3- Bodi ya Wadhamini
b) Vyombo Tendaji
1- Uraisi
2- Afisi ya Katibu Mkuu
3- Kamati za kifundi za kitawi na za kudumu
Sehemu ya Tano: Nguvu na Mamlaka
Kwanza: Jumuiya Kuu
Kifungo [16] Jumuiya Kuu inatmbuka kama mareleleo ya daraja ya juu ya Umoja; na inajuisha wanachama wote waliotajwa katika vipengele (a) na (b) kwenya Kifungo [13] katika katiba hii.
Kifungo [17] Jumuiya Kuu inamiliki mamlaka ya kuwateuwa wanachama wa Mkutano Mkuu kupitia matawi ya Majimbo na ya kitaifa.
Kifungo [18] Jumuiya pekee yake inamiliki haki ya kuuvunja Umoja na hio yataka ridhaa ya thuluthi mbili ya wanachama; na kura zao zinathibitishwa kwa mbinu inaofaa kulingana na maelekezo ya Bodi ya Wadhamini.
Pili: Baraza Kuu
Kifungo [19] Baraza Kuu ndio Mamlaka ya juu anaohusika katika kutunga sera za Umoja na kupitisha mifumo na mikakati yake na kupeana Muelekeo; na Baraza Kuu unafanyika kwa kikao cha kawaida mara moja kila miaka mitano; na inawezekana kufanika katika kikao kisicho cha kawaida kwa mwito wa thuluthi mbili za wanachama wa Jumuiya Kuu au Bodi ya Wadhamini au Afisi ya Raisi.
Kifungo [20] Kwa kumalizika muda wa kikao cha kawaida Jumuiya Kuu, ulio miaka mitano unamalizika muda wa Bodi ya Wadhamini, Afisi ya Raisi na Afisi ya Katibu Mkuu na Kamati zilizoundwa na Jumuiya Kuu.
Kifungo [21] Baraza Kuu unajumuisha wafyatao:
a) Wanachama wote wa Bodi ya Wadhamini, Afisi ya Raisi na Afisi ya Katibu Mkuu na Kamati za kudumu.
b) Mjumbe mmoja kutoka nchi ilio na wanachama wa Umoja
c) Wanachama waangalizi na wanachama wa Heshima ambao Bodi ya Wadhamini inaamua kuwaita; lakini hawa haki ya kupiga kura katika uamuzi wo wote.
Kifungo [22] Maamuzi ya Jumuia yatolewa kwa wingi wa kura za wanachama waliohudhuria isipokuwa kubadilisha katiba ya Umoja ambopo inahitaji umuamuzi wa thuluthi mbili; na iwapo pande mbili zitatoshana basi pande ilio egemea Raisi atapewa ushindi.
Kifungo [23] Baraza Kuu una uwezo na mamlaka ifuatayo:
a) Kuandaa sera za Umoja.
b) Kupitisha na kubadilisha Mkataba wa Umoja
c) Kuchagua na kumuachisha kazi Raisi wa Umoja na Naibu wake na Bodi ya Wadhamini na Katibu Mkuu na Naibu wake na wasaidizi wake na wanachama wa Kamati za kudumu.
d) Kupitisha ripoti za umma na mipangilio ya miaka tano.
e) Kuchukua misimamo ya Umoja katika masuala ya umma.
Tatu: Bodi ya Wadhamini
Kifungo [24] Bodi ya Wadhamini ndio chombo husika katika kufuatilia maaumuzi ya Baraza na mipangilio yake na kuelekeza moja kwa moja vyombo tekelezi na inajumuisha:
a) Raisi wa Umoja na Naibu wake wane.
b) Katibu Mkuu na Naibu wake Wasaidizi wake watano.
c) Maraisi wa Kamati za kudumu.
d) Wanachama sita walioteuliwa na Mkutano Mkuu; na inazingatiwa katika uteuzi wao usawa katika taaluma na mgawanyiko wa kijiografya wa bara hili.
Kifungo [25] Bodi ya Wadhamini itaunda mfumo wake wa utawala katika mkutano wake wa kwanza kwa kuzingatia nyadhifa zifuatazo:
a) Mwenyekiti wa Bodi
b) Naibu wake
c) Karani wa kwanza
d) Karani wa pili
e) Wajumbe; na watagawanyiwa majukumu mengine ambao yanahusu Bodi.
Kifungo [26] ili kuepuka kazi mwingiliano, hakuna mtu kutoka Afisi ya Raisi na Afisi ya Katibu Mkuu atakuwa na haki ya kuwa raisi wa Bodi ya Wadhamini.
Kifungo [27] Bodi ya Wadhamini itafanya mkutano wa kawaida mara moja kila baada ya miezi sita; na inaweza kufanya vikao maalum wakati wowote itajitokeza haja; kwa mwaliko wa Mwenyekiti wake au Raisi wa Umoja au Katibu Mkuu.
Kifungo [28] Bodi ya Wadhamini ina uwezo na mamlaka yafuatayo:
a) Kupitisha kanuni za ndani na kuzibadilisha, na kupitishwa kwa bajeti na ripoti ya kila mwaka iliyotolewa na Afisi ya Katibu Mkuu.
b) kusimamia na kufuatilia kazi ya vyombo tendaji vya Umoja.
c) Uwamuzi wa mwisho wa kupitishwa kwa mikataba na ushirikiano kati ya Umoja na mashirika mengine.
d) Kupitisha kuundwa kwa matawi ya ndani ya nchi na majimboni; na uundaji wa kamati za muda mfupi kwa kazi maalum.
e) uteuzi wa maafisa wa muda kwa ajili ya kujaza nafasi wazi katika vyombo tendaji mpaka wakati wa kikao cha Mkutano.
f) kupitishwa kwa wanachama wapya kwa kuzingatia ridhaa ya Kamati ya Uanachama.
Nne: Afisi ya Raisi
Kifungo [29] Afisi ya Rais wa Umoja ndio marejeleo ya vyombo tendaji, na inajumuisha:
a) Raisi
b) Naibu wa Raisi kwa Afrika Magharibi
c) Naibu wa Rais wa Kanda ya Afrika ya Kati
d) Naibu wa Rais kwa Afrika Mashariki
e) Naibu wa Rais kwa Afrika Kusini

Kifungo [30] inashikilia Afisi Rais kazi na majukumu yafuatazo:
a) Kuwakilisha Umoja katika vyama vingine na kutoa kauli suala kwa niaba ya Umoja katika masuala ya umma
b) Usimamizi wa kazi ya Afisi ya Katibu Mkuu na sekretarieti na Kamati za kifundi.
c) Kuwa mwenyekiti katika vikao vya vyombo tendaji ambazo wanahudhuria na pia mwenyekiti wa kamati za muda mfupi ambazo wao ni wanachama.
d) Kuwa mwenyekiti wa Kamati ya Fatwa
e) Kutia saini kwenye taarifa na makala mbalimbali ambazo zinawasilishwa kwa Mkutano Mkuu
f) Kuitisha Mkutano Mkuu

Kifungo [31] Zitawasilishwa kwa Afisi ya Raisi ripoti zinazotoka kwa Bodi ya Wadhamini na Afisi ya Katibu Mkuu na Kamati.

Tano: Afisi ya Katibu Mkuu

Kifungo [32] Afisi ya Katibu Mkuu ndio tendaji cha Umoja na kinachouwakilisha katika afisi zingine; na inajumuisha:
a) Katibu Mkuu
b) Naibu wa Katibu Mkuu
c) Katibu Mkuu Msaidizi wa masuala ya elimu na utamaduni
d) Katibu Mkuu Msaidizi wa Utawala na Masuala ya Kisheria
e) Katibu Mkuu Msaidizi wa Uhusiano wa Umma na Vyombo vya habari
f) Katibu Mkuu Msaidizi wa Mambo ya Fedha
g) Bi Katibu Mkuu Msaidizi wa Mambo ya Wanawake
Kifungo [33] Katibu Mkuu kwa ridhaa ya Bodi ya Wadhamini, anawateuwa wafanyakazi wanohitajika ili kuendesha kazi; na hasa: Mkurugenzi Mtendaji, Mhasibu, Mweka Hazina

Kifungo [34] Zinatumika Sheria na kanuni za kazi za nchi ya Makao Makuu, kwa wafanyakazi katika Afisi ya Katibu Mkuu.

Kifungo [35] Afisi ya Katibu Mkuu itafanya majukumu na mamlaka zifuatazo:

a) Utekelezaji na kufuatilia maamuzi na mapendekezo ya Baraza Kuu na Bodi ya Wadhamini na kuwasilisha taarifa za mara kwa mara.
b) Kufanya mikataba na ushirikiano na kuiwasilisha kwa Bodi ya Wadhamini kwa ajili ya kupitishwa
c) Usimamizi wa kila siku wa kazi za Umoja na kuziendesha na ufuatiliaji wa kamati kudumu na kamati za muda katika utendaji wa shughuli zake
d) Maandalizi ya mipangilio ya kila mwaka kwa kuzingatia mipango ya miaka mitano na uandalizi wa bajeti ya mwaka na kuziwasilisha kwa ajili ya kupitishwa na Bodi ya Wadhamini.
e) Uandalizi wa ripoti ya mwisho ya kazi ya viungo na vyombo vya Umoja.
f) Maandalizi ya mikutano na kongamano za Umoja.
g) kupendekeza marekebisho ya kanuni za ndani ya Umoja na kuziwasilisha kwa Bodi ya Wadhamini.

Sita: Kamati za Kudumu :

Kifungo [36] Kamati za Kudumu za Umoja ni:
a) Kamati ya Mipango na ufuatiaji
b) Kamati ya Utafiti, Mafunzo na ufasiri
c) Kamati Fatwa na Muongozo
d) Kamati ya Vyombo vya Habari na Uhusiano wa Umma
e) Kamati ya uanachama
f) Kamati ya Fedha
g) Kamati ya Mambo ya Elimu
h) Kamati ya mazungumzo na upatanishi

Kifungo [37] Kila moja ya kamati zilizotajwa inajumuisha mwenyekiti, Naibu wake, Waandishi wawili na wajumbe watano kwa upeo wa juu zaidi.

Sehemu ya Sita:

Kifungo [38] Umoja utafanya juhudi pamoja viungo na vyombo vyake vyote ili kupata mapato ya fedha zinazohitajika kwa kutekeleza mipango na malengo yake; na kufanya bidii katika kukuza mwelekeo wa kujitegemea katika ufadhili; na inaelekeza kwa mapato ya kifedha yafuatayo:
a) Michango ya kila mwaka; na wanawajibika wanachama wote isipo kuwa wanachama waangalizi na wanachama wa heshima; na Bodi ya Wadhamini itaamua kiwango chake.
b) Michango, tunu na wakfu na kadhalika.
c) Uwekezaji na mapato ya machapisho, utafiti na huduma zinazotolewa na Umoja kwa malipo.
d) Mapato mengine yasiogeuka misingi ya Umoja.

Sehemu ya Saba: Hukumu Tofauti Tofauti na Hukumu za Mwisho
Kifungo [39] Inatumika Katiba hii kwa miundo na vyombo vya Umoja vyote pasina kugeuka sheria na kanuni za Nchi yenge makao makuu au matawi yake.
Kifungo [40] Isipokuwa Baraza Kuu, inaweka kufanya mikutano ya viungo na vyombo vyote bila ana kwa ana kwa kutumia mbinu za mawasiliano za sauti na video na mtandao wa kimataifa wa elekroniki kwa kuzingatia kutimiza masharti ya lazima ya mazungumzo ya moja kwa moja, kujadiliana na uamuzi, pamoja na kuzingatia aina ya masuala yanaojadiliwa.

Kifungo [41] Umoja unategemea Kalenda mbili; kalenda ya Kiislamu (kwa kuzingatia kalenda ya Mji wa Mecca) na Kalenda ya Kikristo katika nyakati zake zote; na unazingatia Kalenda ya Kiislamu katika mipangilio yake na nyakati za vikao vya Baraza Kuu.

Kifungo [42] Uanachama wa Umoja wa Wanazuoni wa Afrika na kazi katika viungo na vyombo vyake ni kazi ya kujitolea bila malipo isipokua kwa wale ambao Bodi ya Wadhamini ataamua kuwadumisha kwa ajili ya kazi ya kudumu au kwa muda.

Kifungo [43] Bodi ya Wadhamini itatoa na kupitisha kanuni za ndani za kufafanua hii Katiba kwa kushirikiana na vyombo tendaji katika nyanja husika.

Allah ndiye Mwongozaji kwa njia ilionyoka