Ecrit par & déposé en vertu de غير مصنف.

Kwa Jina la Allah Mwenye Kurehemu Neema Kubwa, Kubwa na Neema Ndogo, Ndogo

Tarehe: 13/04/1435, Sawiya: 13/02/2014 Bayan no: 10
MAUWAJI YA WAISILAMU KATIKA INCHI YA AFRICA YA KATI
Tunamshukuru Allah (sw) Muumba viumbe wote, na twamtakia swala na salamu zimfikie Mtume wetu muongofu na mwenye huruma; Muhammad bin Abdullahi (saw) na Jamaa zake na Maswahaba wake wote: Ama baada ya hayou:
Hakika sisi kama viongozi wa Muungano wa wanavyuoni wakiisilamu wa Africa tumefatiial kwa undani zaidi maovu yanayo tendeka katika inchi ya Africa ya Kati na tukagunduwa uhakika wa mambo haya yakusikitisha:
1. Matatizo ya Africa ya Kati yamebadili mkondo wake na yamekuwa Mauwaji ya kidini yanayo walenga khususa waisilamu ambao ni wananchi na huku ulimwengu ukitazama tu; kama vile inavotukumbusha mauji ya kimbari yaliyo wapaat Watust katika inch ya Ruwanda; Mauwaji ambaoy yametia aibu katika tarekhe ya ubiniadamu ambayo hayatosahulika.
2. Mauwaji haya yakinyama yanafanyika kwa kuwakatakata walio uwawa na vile vile kuwachoma moto maiti katikati ya jiji mbele ya vyombo vya khabari, hata wanawake na watoto wadongo hawakusalimika na uwovu huwo, jambo ambalo lingekuwa bora ni kuwafata majangilu hao na kuwasilisha mahakamani.
3. Kutokana na Majeshi ya Ufaransa kutopokonya silaha majangili hao, na kushindwa kwa majeshi ya Africa, imezidi kuwapa nguvu hao majangili kuendelea na uwovu wao bila khofu yoyote.
4. Msimamo wa viongozi wa kidinin, waisilamu na hata wakiristo ulikuwa wa kuheshimika ijapo uligonga mwamba kutokana na ukosefu wa mafunzo ya kidini na ya kibinadamu wa majangili hao.
5. Umoja wa Nchi za kiafrika umeshindwa kusimamia majukumu yake, na hata umoja wa dola za kimataifa zimezembea katika kupambana na maovu hayo jambo ambalo limepelekea kurudi tena dhulma kama zile zilizo tendeka Rwanda.
6. Hali hii mbaya endapo haitokomwshwa kwa haraka, huwenda ikasambaa na ikasababisha vita vya kidini na vya kimbari katika maeneo mengine jambo ambalo litazidisha matatizo zaidi katika bara zima lilojawa na matatizo.
Hivyo basi Umoja wa wanavyuoni wa Kiisilamu wa Afirika wameamuwa yafatayo:
– Ya kwamba Khutabh zote za ijumaa ya tarehe 21Mfungo Saba 1435/ Sawiya na 21 February 2014 Misikiti yote ya Ijumaa barani Africa na ulimwengu mzima zizungumzie umuhimu wa kuungana na ndugu zetu wa Africa ya kati na kuwaombea Mungu ili usalama na utulivu urudi katika inchi hiyo.
– Kama vile ambavyo tumeamuwa kuweka mpangilio thabiti wa kuwachangia ndugu zetu katika kila inchi ili tuwasaidie waliokimbia mapigano hayo ndani ya inchi na hata inje ya inchi kama wale waliyo kimbilia; Chard, Cameroon, Congo, bila ya kubaguwa dini wala kabil.

Katibu Mkuu wa Muungano                                                                        Raisi wa Mungano
Dr. Said Muhammad Baba Sila                                                                Dr. Said Burhan Abdallah

Laisser un commentaire

Votre adresse de messagerie ne sera pas publiée. Les champs obligatoires sont indiqués avec *