Tamko Nambari: 18 Tarehe 22/11/1438 sawa na tarehe: 14/8/2017
TAMKO LA UMOJA WA WANAZUONI WA AFRIKA KATIKA KULAANI SHAMBULIO LA KIGAIDI MJINI WAGADUGU
Kwa jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehema, Mwenye kurehemu.
Sifa zote njema ni za Mwenyezi Mungu Mola wa viumbe vyote. Na rehema na amani zimfikie Mtume wake Muhammad Bin Abdillah. Ama bada ya hayo:
Kwa hakika, tunafuatilia kwa masikitiko sana msururu wa mashambulizi ya kigaidi yaliyofanyika katika nchi kadhaa katika Pwani na magharibi mwa Afrika, na ambayo la karibuni yake ni shambulizi la kigaidi lililofanyika jioni ya siku ya Jumapili, tarehe 21 Mwezi Mtukufu wa Mfungopili (Dhilqaada), mwaka 1438 sawa na tarehe 13 Agosti 2017 katika mgahawa wa Aziz Istambul, Jijini Wagadugu, Mji Mkuu wa Burkinafaso, lililosababisha vifo vya idadi kadhaa ya watu wa nchi tofauti wasiokuwa na hatia.
Umoja wa Wanazuoni wa Afrika kwa kuzingatia misingi mitukufu ya Uislamu unalaani na kukemea vikali mashambulizi haya, na unakitazama kitendo hiki kama kosa la jinai na dhuluma vyovyote yatakavyokuwa madai ya wenye kuyatekeleza.
Umoja wa Wanazuoni wa Afrika unatoa pole na rambirambi kwa familia za waathirika wa msiba huu na kwa serekali ya Borkinafaso na raia wake; ukitoa mwito wa kusimama pamoja na kuungana baina ya tabaka zote za jamii na nchi ili kusimama imara kwa nguvu moja mbele ya wenye kutekeleza vitendo hivi vya uhalifu kwa ajili kuangamiza uovu wao na kurejesha amani na usalama.
Na mwisho tunaomba Allah kwa msamaha wake na rehema zake aeneze katika jamii zetu neema ya amani, usalama na utulivu.
Tunamuomba Allah amfikishie kwa wingi rehema na amani Mtume wake Muhammad, Jamaa zake na Swahaba wake.
Laisser un commentaire