MUUNGANO WA WANAVYUONI WAAFRIKA MCHAKATO WA MUHULA WA PILI WA MIAKA MITANO.
Kongamano la utukufu wa wakati na mahala, la awamu ya pili la Muungano wa Wanavyuoni Waafrika katika mji mtakatifu wa Makka liliofanywa kwa mda wa siku mbili ndani ya mwezi wa Dhi-hijja tarehe 3 na 4 1439H ikiafikiana na natarehe 14-15 Agosti 2018. Washiriki wa Kongamano hili walikuwa wanavyuoni 205, wote wakiwa wahusika wakuu wa Muungano wa wanavyuoni wa Afrika, washiriki wakiwa ni Maduati, Maimamu, Wasomi na Walimu, Kongamano hili la pili lilikusanya Dola 46 za Afrika za kusini mwajangwa la Sahara, washiriki walifika mji mtakatifu wa Makka kwa usimamizi wa mlinda Misikiti miwili mitakatifu na kwa huduma za Kamati ya Daawa la Afrika na kuna waliofika kwa kupitia mashirika ya Hajj maalumu ya nchi husika.
Kongamano lilianza kwa vikao visivyo pungua saba, kwanza kikao cha ufunguzi kikiongozwa na hotuba ya Raisi wa Umoja wa wanavyuoni wa Afrika Daktari Said Burhan Abdallah, maelekezo ya Kongamano yakatolewa na Katibu mkuu wa Muungano Daktari Said Muhammad Baba Sila, ikifualiwa na hotuba ya msimamzi wa Kongamano uliotolewa kwa niyaba yake na Ustadh Uthman Al-uthman ambaye ndiye katibu mkuu wa Kamati ya Daawa la Afrika.
Kikao chapili cha Kongamano kikafafanua kila aina ya nishati na shughuli zinazofanywa na Muungano wa Wanavyuoni wa Afrika. Ripoti kamili ya fedha ikatolewa inayohusu kipindi cha kumaliza muhula wa kwanza cha uongozi wa Muungano .
Kikao cha tatu cha nne na cha tano Kikahusishwa kutoa maelekezo ya Kamati za kiufundi zikiwemo (Nidhamu asili, mpangilio wa miaka mitano, kamati andalizi ya uongozi ambao utahusishwa na kuchaguwa majina ya wanachama wa Muungano watakao ongoza katika muhula mpya.
Kikao cha sita kikahusishwa kwa kutolewa ripoti maalumu za kazi za kamati tatu za kiufundi na kutolewa pia mapendekezo yanayohusu mabadiliko katika Sharia za Muungano na miradi pendekezwa inayohusu mipangilio ya miaka mitano ya uongozi, pia ikihusisha majina ya wagombea walio wanachama kwa ofisi mpya.
Ripoti zote zikapitishwa na kukubaliwa kwenye mkutano mkuu wa kongamano.
Kikao cha saba kikawa ni cha kufunga kongamano, kukiwa na uhudhuriaji mkubwa wa wanachama, kwenye kiako hiko ikasomwa taarifa ya kufunga kikako na kufuatiliwa na hotuba ya Raisi wa Muungano aliyechaguliwa kwa uongozi kwa mara ya pili, kisha ikafuatiliya hotuba ya msimamizi wa Kongamano Al- amir Daktari Bandar bin Salman bin Muhammad Al-suud ambaye ni Raisi wa Kamati ya Da-awa Afrika, Kisha ikafuatiliya hotuba ya Rais wa Kongamnao Ustadh Daktari Muhammad Ahmad Loh, na ikafuatiliya hotuba ya mgeni wa heshima Abdurahman Assudeisi ambaye ndie kiongozi mkubwa wa Misikiti miwili mitukufu Msikiti wa Haran na Msikiti wa Mtume Muhammad, naye mgeni wa heshima akafunga kikao kwa kusoma aya za Quran takatifu.
Kwa maelezo haya kuliafikiwa kuwaongezea mda wa uongozi Raisi wa Muungano Daktari Said Burhani Abdallah na Raisi wa bodi ya wakurugenzi Muhammad Ahmad Loh na Katibu mkuu Said Muhammad Baba Sila na wengi katika viongozi waliopita wa Muungano wakiongozewa mda wao.
Matumaini mengi yamefungamanishwa na washika ofisi mpya likiwa jukumu lao ni kuhakikisha ujumbe wa Muungano katika muhula mpya ambao umebeba ujumbe maalumu ” kuboresha juhudi za Wanavyuoni Afrika na kuunganisha safu zao ili kuongoza Umma katika muongozo wa Uislamu ulio sahihi” kwa Idhini ya Allah aliye tukuka naye ndiye mwenye kututosheleza kwa kila jambo, na kwa Mtume mtukufu salamu na sala ziwe juu yake.
Laisser un commentaire