Ecrit par & déposé en vertu de غير مصنف.

Tamko Na.: 22                                                                      Tarehe: 13/05/1440= 19/01/2019

TAMKO LA UMOJA WA WANAZUONI WA KIISLAMU WA AFRIKA LA KULAANI SHAMBULIZI LA KIGAIDI LA NAIROBI

KWA JINA LA ALLAH MWINGI WA REHEMA, MWENYE KUREHEMU

Shukurani anazistahiki Allah Mola wa viumbe, na rehema na amani zimfikie Mtume wake Muhammad Bin Abdallah, Familia yake na Swahaba wake wote.

Umoja wa Wanazuoni wa Kiislamu wa Afrika umefuatilia kwa masikitiko na huzuni matukio ya shambulizi la kigaidi liliolenga jengo lenye hoteli na ofisi katika Mji Mkuu wa Kenya Nairobi na ambalo lilitokea siku ya Jumanne tarehe 15 Januari 2019 sawa na 09 Mfunguonane 1440 na ambalo limesababisha makumi ya watu kuuawa na kujeruhiwa.

Kwa kutekeleza wajibu wake wa kidini na wa kibinadamu, Umoja wa Wanazuoni wa Kiislamu wa Afrika unatangaza yafuatayo:

  1. Umoja wa Wanazuoni wa Kiislamu wa Afrika, kwa kuegemea kwenye misingi ya dini ya Kiislamu inayokataza kuua watu wasiokuwa na hatia, unalaani shambulio hili la kigaidi.

  2. Umoja wa Wanazuoni wa Kiislamu wa Afrika unatoa pole kwa familia za waathirika na kwa taifa la Kenya, na unawaombea majeruhi wapone haraka.

  3. Umoja wa Wanazuoni wa Kiislamu wa Afrika unayaomba makundi yote ya jamii ya Wakenya kuungana katika kuukabili ugaidi kwa aina zake zote, ugaidi ambao hauna dini wala rangi.

  4. Umoja wa Wanazuoni wa Kiislamu wa Afrika unatoa wito kwa watu wenye busara na ushawishi, taasisi na serikali kufanya juhudi za ziada ili kumaliza migogoro iliyotapakaa katika bara la Afrika na ambayo magaidi wananufaika nayo na wananchi kwa daraja la kwanza ndio wanaoathirika.

Mwisho, tunamuomba Allah kwa rehema zake azipe jamii zetu amani na utulivu.

Tunamuomba Allah amfikishie rehema na amani nyingi  Mtume wetu Muhammad, Familia yake na Swahaba wake.

 

Dkt. Said Mohamed Babasila          Dkt. Said Burhan Abdallah

 

Katibu Mkuu                                Rais wa Umoja wa Wanazuoni wa Kiislamu wa Afrika   

 

Laisser un commentaire

Votre adresse de messagerie ne sera pas publiée. Les champs obligatoires sont indiqués avec *