WITO WA AMANI KATIKA MWEZI MTUKUFU WA RAMADHAN 1440/2019
Wito wa amani – Kusitisha aina zote za vita wakati wa mwezi mtukufu wa Ramadan 1440 AH / 2019
Kwa jina la Allah mwingi wa rehema mwenye kurehemu. Sifa njema zote ni za Allah na sala na amani ziwe juu ya Nabii wa huruma Muhammad bin Abdullah na familia yake na Maswahaba. Baada ya hayo:
Wamepitia mateso mengi watu katika nchi za ukanda wa pwani wa Afrika na zile za pembe ya Afrika kusini jangwa la sahara, na bado wanaendelea kuteseka kutokana na migogoro ya kivita ambayo imesabibisha vifo vya maelfu ya watu, kuharibiwa kwa mali, kufurushwa mamia na maelfu ya watu kutoka katika makazi yao na kutowesha utulivu na amani. Na kwa kuwa wengi wa watu wa eneo hili ni Waisilamu na wao wamekaribiwa na mwezi mtukufu wa Ramadhani ambao ni mtukufu kwao na kwa wengine pia. Ili kupunguza mateso na kufungua matumaini ya amani, Umoja wa wanavyuoni wa Afrika, na wanachama wa umoja huo kutoka nchi 46 za Afrika kusini jangwa la sahara, wanatoa ombi lifuatalo kukomeshwa kabisa kwa vita wakati wa mwezi mtukufu wa Ramadhani kupitia vipengele vifuatavyo:
– Wito kwa vyama vyote vya nchi za ukanda wa pwani ya Afrika na zile za pembe ya Afrika kutoka majeshi ya nchi, vikosi vya kimataifa na vikosi vya wanamgambo bila ubaguzi.
– Kuwajumuisha wote kwenye harakati za kuleta usalama kwa kuacha vita katika mipaka yote katika nchi za ukanda wa pwani wa afrika na zile za Pembe ya Afrika wakati wa mwezi mtakatifu wa Ramadan (5 Mei hadi 4 Juni 2019).
– Ushiriki wa makundi yote ya jamii, hasa viongozi wa kidini na wa jadi, katika kukuza wito huu kwa kutekeleza na kuufuata.
– Kutumia nafasi ya mkataba huu wa kusimamisha vita katika mwezi huu mtakatifu kuandaa majadiliano ya pamoja bila kumbagua yeyote katika ngazi zote na kujadili njia za kutatua migogoro na kuleta amani na utulivu.
– Kuundwa kwa kamati za juu zitakazo jumuisha viongozi wa dini na jamii zitakazo shughulikia mambo ya manufaa kwa jamii na usuluhishi ili kufikia upatanisho kati ya vyama.
– Kutumia nafasi hii ya makubaliano ya kusimamisha vita wakati huu wa mwezi mtakatifu kuzingatia mazungumzo mazuri kati ya serikali na vikundi vya wanamgambo kwa njia tofauti ili kufikia makubaliano ambayo yatasitisha umwagikaji wa damu na kuregesha amani na maendeleo.
– Kuimarisha wito wa kufanikiwa kwa mkataba ili kufikia amani ya kudumu ili watu wapate kuishi katika usalama na ustawi.
Laisser un commentaire