Ecrit par & déposé en vertu de غير مصنف.

TAMKO NAMBARI 24    Tarehe 30/3/1441 Hijiria 28 /11/2019 Miladia

TAMKO LA JUMUIYA YA WANAVYUONI WA AFRIKA LINALO TOA WITO WA KUKATAZA KUTUMIA NENO “MUJAHIDINA” KWA MAKUNDI YANAYO BEBA SILAHA

Himdi zote ni za Allah. Swala na salamu zimuendee Nabii wa uongofu na wa rehema, Muhammad Bin Abdallah pamoja na Swahaba zake.
Baada ya utangulizi:
Hakika, Jumuiya ya Wanavyuoni wa Afrika imeshuhudia wakati huu wa sasa kutumika kwa wingi na kwa kupita kiasi neno “Jihadi” kwa matendo ya kihalifu pia kutumiwa neno “Mujahidina” kwa makundi yenye kubeba silaha yanayo fanya vitendo hivyo, na hasa utumiaji huu ukifanywa na vyombo vya habari na baadhi ya viongozi katika maeneo kadhaa ya Afrika.
Hakika, Jumuiya ya Wanavyuoni wa Afrika, kwa kuzingatia wajibu wake, inatoa wito wa kuacha kabisa kutumia neno “Jihadi” kwa operesheni za kihalifu au kutumia neno “Mujahidina” kwa makundi yenye kubeba silaha yanayofanya operesheni hizo zilizoenea sehemu kadhaa za Afrika na nchi nyinginezo, hasa nchi za ukanda wa Pwani na Pembe ya Afrika. Wito huu uyafikie makundi yote ya wanajamii katika nchi hizo na nyinginezo, na hasa viongozi, waandishi wa habari, wasomi na makada wa makundi ya kijamii.
Wakati Jumuiya ya Wanavyuoni wa Afrika ikikataa kutumiwa kwa msamiati wa “Jihadi” kwa vitendo hivyo vya kihalifu inaegemea kwenye hoja zifuatazo:-
• Kutumia neno “Jihadi” kwa vitendo vya kihalifu au neno “Mujahidina” kwa makundi yanayo fanya vitendo hivyo, ni kuukosea Uislamu kwa kukusudia au kwa kutokukusudia, kwa sababu ni jambo linalo julikana kwamba msamiati wa “Jihadi” unahusu ibada ya Kiislamu yenye vigezo vyake, masharti yake na hadhi yake katika maandiko ya Kiislamu na pia ibada hiyo ina uwanda wake mpana katika historia ya Uislamu.
• Kutumia neno “Mujahidina” ni kuyapa nguvu, kwa kukusudia au kwa kutokusudia, makundi hayo yanayofanya vitendo hivyo vya kihalifu.
• Kuyapa msamiati wa “Mujahidina” makundi hayo ya kihalifu kuna athari hasi kwa vijana wenye ufahamu mdogo wa sheria za Kiislamu kiasi kwamba wanashawishika kujiunga na makundi hayo au wao wenyewe binafsi kufanya vitendo hivyo vya kihalifu.
• Mwisho: Ikiwa ni muendelezo wa matamko yaliyo pita, Jumuiya ya Wanavyuoni wa Afrika inatoa wito wa

kuunganisha nguvu ili kuziangamiza sababu za fitina na machafuko ili amani na usalama urudi katika jamii zetu. 

Swala na salamu zimuendee Mtume Muhaamad s.a.w.

            Katibu Mkuu                               Raisi wa Jumuiya ya Wanavyuoni wa Afrika

Dr. Seydou Madibaba SYLLA                             Dr. Said Bourhani Abdallah

Laisser un commentaire

Votre adresse de messagerie ne sera pas publiée. Les champs obligatoires sont indiqués avec *