Ecrit par & déposé en vertu de غير مصنف.

18/8/1443 AH / 3/21/2022 AD

MWITO WA MWEZI MTUKUFU WA RAMADHANI 1443 AH 2022 AD

 

MWITO WA KUONDOSHWA VIKWAZO DHIDI YA NCHI YA MALI; NA MAPATANO YA KUSITISHA MAPIGANO NA KUFANYIANA UADUI KATIKA MWEZI MTUKUFU WA RAMADHANI 1443 AH / 2022 AD, HASA KATIKA MAENEO YENYE MIGOGORO KATIKA AFRIKA YA KUSINI JANGWA LA SAHARA.

 

Kwa Jina la Mwenyezimungu Mwingi wa Rehema Mwenye Kurehemu

Wakuhimidiwa ni Allah sala na salamu zimuendee mtume wake wa rahma Muhammad mtoto wa Abdillahi pamoja na Ahli zake na Swahaba zake.

 

Baada ya salamu: Waanza mwezi mtukufu wa Ramadhani mwaka huu tarehe 2 Aprili 2022 A.D (ikitegemea mwandamo wa mwezi), kwa mda wa mwezi mmoja Waislamu watakuwa kwa saumu pamoja na ibada nyinginezo, kuna Waislamu katika nchi zote za Afrika Kusini Jangwa la Sahara kwa viwango tofauti tofauti; Ramadhani ni mwezi mtukufu kwao, na mwezi wenyewe huheshimiwa pia na wasiokuwa Waislamu.Kwa hivyo, Umoja wa Wanavyuoni wa Afrika, pamoja na wanachama wake kutoka nchi 47 za Afrika, wanatoa mwito unaoitwa mwito wa Ramadhani tukufu 1443 AH / 2022 AD; umoja wa Wanavyuoni huu unamaombi mawili:

Ombi la kwanza:

 

Twaomba viongozi wa Jumuiya za Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi kusitisha vikwazo vilivyoekewa Nchi ya Mali na kundi maalumu hasa wakati wa mwezi wa Ramadhani; vikwazo hivyo vikiondoshwa itakuwa afueni kwa watu wa Nchi ya Mali na raia wa nchi za eneo lililoathiriwa na vikwazo hivyo; Umoja waWanavyuoni unataka iongezwe juhudi maradufu za kufikia suluhu ya kudumu katika mwezi huu wa Ramadhani kwa kuondolewa  kabisa vikwazo ilivyoekewa  nchi  ya Mali na nchi iweze kuendelea na njia zake  za maendeleo.Barua za ombi hili zimetumwa kwa wakuu wote wa nchi za Jumuiya za Kiuchumi za Afrika Magharibi (ECOWAS/SEDIAW).Ombi la piliWito  kwa pande zote zenye migogoro katika nchi za kanda mwa Bahari na ziliopo katika pembe ya afrika ya kati, ikijumuisha majeshi ya nchi, vikosi vya kimataifa, vikundi vyenye silaha na wanamgambo wanaobeba silaha, bila ubaguzi, kutii makubaliano ya amani na kusitisha vita na mapigano, katika kipindi hiki cha mwezi mtukufu wa Ramadhani; ni muhimu wasisitize wito huu viongozi wa dini, na viongozi wa kijamii, pia ni muhimu kutafuta suluhu ya kudumu  ya migogoro inayoendelea ambayo imesababisha watu  wengi kuteseka kwa muda mrefu.

 

Tunamuomba Mwenyezimungu aziafikie juhudi zote zinazofanywa za kumaliza migogoro hii ambayo imeongeza huzuni na mateso kwa watu wasiokuwa na hatia .

 

 

Laisser un commentaire

Votre adresse de messagerie ne sera pas publiée. Les champs obligatoires sont indiqués avec *