Tamko la Muungano wa wanazuoni wa Afrika kuhusu Uamuzi wa Rais wa Merikani Donald Truph kuhamishia ubalozi wa Merikani Jijini Jerusalemu.
Sifa zote njema ni za Allah Mola wa viumbe vyote and rehema na amani zimfike bwana Mtume wa Allah na ahli zake na maswahaba wake wote; baada ya hayo:
Anasema Allah Mtukufu aliye tukuza {Ametukuza Mola aliempeleka mja wake usiku kutoka msikiti mtukufu wa Maka mpaka msikiti wa Jerusalemu abao tumebariki pembeni mwake}
Kwa kuambatana na ujumbe wa muungano wa wanazuoni wa Afrika na kujihusisha na masuala ya waislamu kwa hakika tunatangaza kulaani kwetu kwa ukali uamuzi wa Rais wa Merikani kuhamisha ubalozi wa Amerika kuupeleka Mashariki mwa Jijini Jerusalemu lilokaliwa kimabavu na unatazama hii hatua ni kama kutangaza malumbano ya kiwazi na uadui wa wazi kwa maeo matakatifu ya maislamu kwa ajili ya kuwachokoza hisia za bilioni moja na nusu ya waislamu Ulimwenguni. Na Muungano unasisitiza kwamba hii hatua inaothibiti ukalizi wa kimabavu sisi waislamu hatutakubali na ni wajibu wetu wa kidini kubainisha haki na kutonyamaza
Muungano unatoa mwito kwa watu wa Palestani wa tabaka zao na makundi yao kwa muelekeo unaowajibika ili kupambana na mabadiliko ya hatari na waendeleze mapambano yao na kupinga kwao ukalizi wa kimabavu na sera zakujipanua na Muungano unatangaza kuungana mkono na kusimama sambamba waislamu wa Afrika pamoja na mapambano ya kitaifa wa Palastina na unawataka waislamu wote ulimwenguni kuchukua mwelekeo wa kulaani uamuzi huu wa kidhuluma ili kunisuru Mji wa Jerusalemu na Msikiti mtukufu wa Aqsa na kuunga mkono Palestina na haki za wananchi waki kuwa na uhuru na kujisimamia na kufukuza ukoloni wa kiisraeili na kuupinga.
Na unaomba viongozi na marais wa nchi za kiarabu na kiislamu kusimama pamoja msitari mmoja kupinga upinga uamuzi huu kwa mbinu zote zinazowezekana na halali na kunataka serekali za nchi za kiarabu kuchukua misimamo ya wazi ili kuulinda Msikiti wa Aqsa na kutoshiriki katika masungumzo au mapatano yanao timiza kuachilia Jerusalemu au sehemu ye yote ya Palestina.
Na Muungano unatoa wito kwa wizara za wakfu katika nchi za kiarabu na kiislamu ili kufanya misikiti na khutba za kidawa ili kuelimisha watu kuhusu maswala ya Palestina na Jerusalemu na kusimama na pamoja na ndugu zetu Jerusalemu, na kubainisha umuhimu wake katika sheriah, na hatari ya hatua za kuufanya ya Kiyahudi. {Enyi watu walioamini subirini na mjisubirishe na msimame kideti na muogope Allah ili mufahaulu}. Na amesema Mtukufu wa Enzi {Sisi tunawasuru watume wetu na walioumini katika maisha ya duniani na siku ambao watasimama mashahidi}
Na Allah ampe rehema na amani bwana wetu Muhammad na ahli zake na maswahaba zake.
Katibu Mkuu Rais Muungango wa wanazuoni wa Afrika.
Laisser un commentaire