Tamko Na.: 22 Tarehe: 13/05/1440= 19/01/2019
TAMKO LA UMOJA WA WANAZUONI WA KIISLAMU WA AFRIKA LA KULAANI SHAMBULIZI LA KIGAIDI LA NAIROBI
KWA JINA LA ALLAH MWINGI WA REHEMA, MWENYE KUREHEMU
Shukurani anazistahiki Allah Mola wa viumbe, na rehema na amani zimfikie Mtume wake Muhammad Bin Abdallah, Familia yake na Swahaba wake wote.
Umoja wa Wanazuoni wa Kiislamu wa Afrika umefuatilia kwa masikitiko na huzuni matukio ya shambulizi la kigaidi liliolenga jengo lenye hoteli na ofisi katika Mji Mkuu wa Kenya Nairobi na ambalo lilitokea siku ya Jumanne tarehe 15 Januari 2019 sawa na 09 Mfunguonane 1440 na ambalo limesababisha makumi ya watu kuuawa na kujeruhiwa.
Kwa kutekeleza wajibu wake wa kidini na wa kibinadamu, Umoja wa Wanazuoni wa Kiislamu wa Afrika unatangaza yafuatayo:
-
Umoja wa Wanazuoni wa Kiislamu wa Afrika, kwa kuegemea kwenye misingi ya dini ya Kiislamu inayokataza kuua watu wasiokuwa na hatia, unalaani shambulio hili la kigaidi.
-
Umoja wa Wanazuoni wa Kiislamu wa Afrika unatoa pole kwa familia za waathirika na kwa taifa la Kenya, na unawaombea majeruhi wapone haraka.
-
Umoja wa Wanazuoni wa Kiislamu wa Afrika unayaomba makundi yote ya jamii ya Wakenya kuungana katika kuukabili ugaidi kwa aina zake zote, ugaidi ambao hauna dini wala rangi.
-
Umoja wa Wanazuoni wa Kiislamu wa Afrika unatoa wito kwa watu wenye busara na ushawishi, taasisi na serikali kufanya juhudi za ziada ili kumaliza migogoro iliyotapakaa katika bara la Afrika na ambayo magaidi wananufaika nayo na wananchi kwa daraja la kwanza ndio wanaoathirika.
Mwisho, tunamuomba Allah kwa rehema zake azipe jamii zetu amani na utulivu.
Tunamuomba Allah amfikishie rehema na amani nyingi Mtume wetu Muhammad, Familia yake na Swahaba wake.
Dkt. Said Mohamed Babasila Dkt. Said Burhan Abdallah
Katibu Mkuu Rais wa Umoja wa Wanazuoni wa Kiislamu wa Afrika
Laisser un commentaire